Malaria Yatajwa Kupungua Malindi
Usimamizi wa hospitali ya kaunti ndogo ya Malindi kaunti ya Kilifi sasa Umebainisha kuwa visa vya ugonjwa wa Malaria vimepungua kwa asilimia kubwa kule Malindi katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita.
Kulingana na Afisaa msimamizi wa afya kaunti ndogo ya Malindi Evance Ogato maambukizi ya Malaria kaunti ndogo ya Malindi yamepungua kutoka asilimia 40 hapo awali hadi asilimia tano hivi sasa.
Afisa huyo anasema kuwa maeneo mengi ya kaunti ya Kilifi maambukizi ya malaria yamepungua isipokuwa sehemu kama Kilifi Kazkazini na Ganze ambako visa hivyo vingali vinapatikana.
Ogato anahoji kuwa ugonjwa huo kwa sasa sio hatari tena ikilinganishwa na viwango vya maambukizi ya awali hii ni kutokana na juhudi kambambe za wizara ya afya.