Makundi haramu yaonywa kwale.

Gavana wa Kwale Salim Mvurya amelaani vikali mchakato wa kuanzishwa kwa makundi ambayo yamekuwa yakilenga kuchangia ukabila na kutatiza uwiano wa wakazi wa eneo hilo.

Akizungumzia kundi la Utsi linalokisiwa kuwa na njama fiche ya kuwakandamiza wakazi katika Kaunti hiyo ambao si Wamijikenda, Mvurya amesema kwamba kamwe serikali yake haitaruhusu hilo kufanyika.

Kwa mjibu wa Mvurya makundi hayo yamechochewa na wanasiasa ambao wamekuwa wakiupinga uongozi wake.

Tarehe kumi na mbili mwezi huu kundi hilo ambalo lilianzishwa na baadhi ya wazee wa kabila la Digo lilisema kwamba lengo lake ni kuhakikisha jamii ya Mijikenda inapata fursa ya uongozi katika serikali ijayo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *