Makavazi ya forty jesus yalindwe.

Usimamizi wa makavazi ya Fort Jesus unasema unajitahidi kulinda historia kwa ajili ya kuhamasisha wanafunzi na hata watalii wanaozuru eneo hilo.

Afisa mkuu wa makavazi hiyo Fatma Twahir anasema licha ya makavazi ya Fort Jesus kujengwa karne nyini zilizopita, kuna haja ya eneo hilo linalotambulika kimataifa kutokana na historia yake kulindwa.

Twahir anasema kumekuwa na changamoto ya baadhi ya wanafunzi wanaotalii eneo hilo na kuweka michoro ambayo haiambatani na maudhui ya makavazi hiyo.

Jengo hilo lilifunguliwa rasmi kwa umma baada ya kufungwa kwa mda wa miezi sita kutokana na maambukizi ya covid 19.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *