Makali ya COVID 19 dhidi ya Uchumi wa New Zealand

New Zealand inakumbwa na hali ngumu ya kiuchumi kufuatia maagizo makali yaliowekwa  kukabiliana na maambukizi ya virusi vya Corona nchini humo.Pato la jumla nchini humo lilipungua kwa kiwango cha asili mia 12.2% kati ya miezi ya Aprili na june wakati wa uterkelezaji wa maagizo hayo makali.Hi ni mara ya kwanza kwa New Zealand kukumbana na hali hiyo tangu mzozo mkubwa wa kifedha wa kimataifa wa mwaka 1987.Lakini serikali ya nchi hiyo inatumai hatua ilizohukua kukabiliana na janga hilo zitachochea ufufuzi wa kiuchumi nchini humo.Taifa hilo la takriban watu milioni tano wakati mmoja lilitangaza kukabili  virusi hivyo,ingawaje bado kuna visa vichache vya maambukizi ya Corona na imenakili vifo 25 kutokana na maambukizi hayo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *