Makabiliano dhidi ya Corona,tahadhari yatolewa

Watu wanaogua maradhi mbalimbali Kama ya figo wameshauriwa kufuata maagizo yote ya kujikinga na maambukizi kwani ni miongoni mwa watu walio katika hatari kubwa ya  kuambukizwa ugonjwa wa covid19.

Kulingana na muuguzi anayeshughulikia wagonjwa wa figo katika hospitali ya rufaa ya Moi mjini Voi Lucy Nyata,wagonjwa wa figo kinga yao ya mwilini huwa chini hali inayowaweka katika hatari kubwa zaidi.

Kadhalika Nyata amebainisha kuwa magonjwa ya kisukari na shinikizo la damu huchangia kupata magonjwa ya figo.

Aidha Nyata ameshauri wagonjwa wa figo kuzingatia lishe bora ili kupata kinga bora mwilini sawa na kuzingatia kliniki pamoja na kutumia dawa kama wanavyoagizwa na madaktari. �>4zבm

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *