Maisha yangu si feki

Mbosso Khan,msanii toka kundi la WCB anayetamba kwa kazi yake mpya sina nyota'wimbo unaofanya vizuri sana pande za YouTube, kadokeza mengi ndani ya TSA akifanya mahojiano na Gates Mgenge,tukiacha usanii Mbosso ana familia inayo mtegemea ndo maana juhudi zake anapambana sana,mimi siishi maisha feki vile unaniona niko vile ata tukikutana,gari lisemekanalo ni la Tanasha sikweli lile ni gari langu mwenyewe, niliwanunulia nyumba wazazi wangu,gari pia nami pia nikajizawadi mwenyewe,sio mrahisi wa kufanya collabo na tukifanya basi ujue nimekuheshimu,mmoja ya watu nliofanya nao kazi bila kusukumana wala nini ni msanii Susumila toka Mombasa Kenya, uhusiano wangu na Joho uko sawa ni rafiki yangu,kakangu namheshimu sana,kipato changu kupitia YouTube sio nyingi vile ila ni hela ambayo yanikimu mahitaji yangu nashukuru,mtoto wangu nilozaa nae na mwanamke kutoka mombasa naishi nae huku Tanzania kwa kua mamake keshaoleka kwengine ila tunaongea, maudhui ya wimbo wangu wa sina nyota umefanya watu wanishauri niingie katika ulingo wa uigizaji hivo basi watu watarajie kuona kazi tuu,kikubwa zaidi watu wasubirie Album yangu mpya ya kwanza kabisa kutoka kwangu katika maisha ya mziki,nawapenda sana mashabiki wangu watarajie makubwa,kwetu Tanzania mziki umepewa nafasi kubwa yaani unazingatiwa zaidi ndo maana tunasikizwa sana,vile vile pia mimi sija mfukuza meneja wangu tulikosa tuu maelewano kikazi,ila kwa sasa sina meneja’.~Mbosso Khan

SHUKRAN :Tizo Waleo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *