Mahakama yalaumiwa kwa utepetevu

Idara ya mahakama nchini imelaumiwa vikali kutokana na hatua yake ya kuchelewesha uamuzi wa kesi nyingi zinazowasilishwa mahakamani  hatua iliyotajwa kulemaza shughuli za serikali nchini.

Akizungumza wakati alipozuru afisi za uvuvi kule Malindi waziri wa kilimo , uvuvi na utsawi wa mifugo Peter Munya amesema kuwa maeneo mengi ya uvuvi  nchini yamenyakuliwa na mabwenye huku kesi zilizowasilishwa dhidi ya maeneo hayo ya uvuvi zikisalia mahakamani bila kutatuliwa kwa muda ufaao.

Munya amesema kuwa mabwenyenye huonyesha uwezo wao mahakamani huku mwamanchi akikosa haki hatua ambayo ameikashifu vikali.

Aidha amesema kuwa ripoti ya BBI sharti iangazie hata Zaidi idara ya mahakama jinsi inavyoingilia miradi ya serikali na  badala yake kuitaka idara hiyo kuwa huru.

Wakati huo huo  amesema kuwa  serikali itafanya kila liwezekanalo kuhakikisha kuwa kuwa maeneo yote ya uvuvi yaliyonyakuliwa na mabwenyenye yanaregeshwa kwa wakazi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *