Magoha, masomo Yote Mwakani

Waziri wa elimu Profesa George Magoha ametangaza vyuo vikuu vyote kufunguliwa Januari 2021.

Hatua hiyo imejiri baada ya kubainika kuwa vyuo havijaweza kuweka mikakati madhubuti inayohitajika kuambatana na muongozo wa wizara ya afya kudhibiti maambukizi ya Covid 19.

Katika taarifa kwa waandishi wa habari Profesa Magoha amesema uchunguzi wao umebaini kuwa ni asasi chache mno zilizochukua hatua stahiki za kuwalinda wanafunzi, wahadhiri na wafanyakazi wengine wa vyuo dhidi ya virusi vya Corona.

Mapema mwezi huu, wizara ya elimu ilikuwa imetangaza kuwa vyuo vingefunguliwa tena mwezi Septemba mwaka huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *