Magoha Azuru Pwani

Waziri wa elimu prof.George Magoha anatarajiwa kuzuru kaunti mbili za pwani leo asubuhi ili kutathmin hali ya masomo shuleni sawia na mazingira ya shule.

Saa mbili na robo atafanya kikao na wadau wa elimu akiwemo afisa mkuu wa elimu,afisa mkuu watume ya kuwajiri wa tsc,na wakuu wa usalama katika kaunti ya kilifi kwenye ofisi ya kamishna wa kaunti hiyo kisha kuzuru shule ya msingi ya kilifi saa tatu na robo.

Ziara sawia na hiyo ataifanya katika kaunti ya Mombasa saa tano asubuhi katika ofisi ya kaunti kamishna,ambapo anatarajiwa kukutana na wakuu wa elimu sambamba na wale wa usalama kisha majira ya saa sita mchana atazuru shule ya upili ya wasichana ya Al-Farsi,kabla ya kuwahutubia wanahabari saa saba mchana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *