Ligi Ya Kenya Yapata Nuru

Sasa ni habari njema kwa ligi kuu ya FKFPL humu nchini hii ni baada ya shirika la habari la StarTimes kuingia kwenye mkataba wa miaka saba na shirikisho la soka la FKF  ili kuonyesha mbashara mechi za ligi kuu nchini, ligi ya wasichana, mechi za timu ya taifa Harambee stars pamoja na ligi ya daraja la chini la NSL.

Habari hii njema imethibitishwa ni rais wa shirikisho la soka Nick Mwendwa pamoja na shirika hilo la habari.

Akiweka wazi taarifa hio Mwendwa amesema kila mwaka ligi itapata ufadhili wa dola milioni 1.1 ambazo ni sawa na shilingi miioni 119,284,000.00 za Kenya.

Wakati huo huo vilabu vyote vinavyoshiriki mechi mbali mbali za ligi nchini vitaweza kupewa ufadhili wa mipira kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa mwaka 2020/2021.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *