Lalama Za Wazazi Malindi

Wakazi kaunti ya kilifi wamepinga vikali Kauli ya waziri wa elimu Prof.George Magoha kuwa wanafunzi wafunjwe nje ama chini ya miti kama njia moja wapo yakusaidia msambao wa virusi vya Corona.

Wakizungumza mjini kilifi Wakazi hao wameeleza kugadhabishwa kwao na jambo hilo wakisema kuwa watoto wako katika hatari kubwa yakuumwa na wadudu na kushikwa na magojwa kama malaria kwa kuumwa na mbu.

Wakiongozwa na Willy Mele wamesema kuwa kila mtoto ana haki yakusoma katika mazingira mazuri ili waweze kumakinika  kikamilifu Wakati wanapo funzwa.

Aidha wamesema wanafunzi wanaosoma nje ya madara wanakumbwa na changamoto nyingi ikiwemo ukosefu wa vitu muhimu kama ubao(black board), Teaching Aids na nyinginezo nyingi.

Wakazi hao wameitaka serika ya kitaifa kuja na mbinu badala kuhakikisha kuwa wanafunzi wanasoma katika mazingira mazuri.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *