Lalama Za Madereva Wa Masafa Marefu

Chama cha madereva wa masafa marefu kimeitaka serikali kupitia wizara ya afya kuweka wazi suala la upimaji wa madereva katika kituo cha Miritini Inspection.

Akiongea katika eneo hilo ambapo Zaidi ya madereva 200 walikusanyika kwa ajili ya kupata vipimo vya Covid-19,katibu mtendaji wa chama hicho Masoud Mwatela amesema kuna baadhi yao wamekuwa hapo kwa siku tatu bila kupata huduma hiyo.

Kauli yake imetiwa mkazo na mwenyekiti wa madereva hao Roman Waema akidai kuipeleka serikali mahakamani kwa kukiuka haki za madereva nchini.

Kwa upande wao madereva hao wakiongozwa na Anthony Mwangi amesema kuwa madereva wengi hawawezi kuingia bandarini kwa sababu vyeti vyao vimeisha muda.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *