Kutoshirikiana ndio chanzo cha kukosa maendeleo eneo la Pwani

Ukosefu wa ushirikiano mwema miongoni mwa viongozi wa Pwani ni mojawapo ya changamoto inayolemeza juhudi za kutafuta suluhu ya matatizo ya wapwani.

Haya ni kwa mjibu wa seneta wa kaunti ya Taita Taveta Johnes Mwaruma anayeungama kuwa ukosefu wa umoja pia umechangia kusambaratika kwa vyama vingi vya kisiasa mkoani  Pwani hali inayosababisha mkoa huo kuendelea kusalia nyuma kimaendeleo.

Aidha amekiri kuwa kuna majadiliano miongoni mwa viongozi wa Pwani kuunda chama kimoja cha kisiasa japo lazima wapate maoni ya wakaazi wa Pwani kabla ya kutekeleza wazo hilo.

Haya yanajiri baada ya baadhi ya maseneta na wabunge wa Pwani kutishia kuzindua  chama kipya kinachochazamiwa kutumika mwaka wa 2022.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *