Kumi zaidi wafariki kutokana na covid19 nchini

Wizara ya afya ilitangaza visa 604 zaidi vya maambukizi ya ugonjwa wa COVID-18 hapa nchini na kufikisha idadi jumla ya visa vya maambukizi kuwa 42,541.

Kwenye taarifa, waziri wa afya, Mutahi Kagwe, alisema visa hivyo vipya vilithibitishwa kutoka kwa sampuli 5,832 zilizopimwa katika muda wa saa 24 zilizopita.

Watu 88 walipona ugonjwa huo, huku Idadi ya vifo kutokana na ugonjwa huo ikifikia watu 797 baada ya wagonjwa 10 kuaga dunia kutokana na ugonjwa huo.

PICHA KWA HISANI

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *