Kizaazaa mahakamani Mombasa,kulikoni?

Kulikuwa na kizaazaa kwenye mahakama moja ya Mombasa baada ya mfungwa mmoja kuzua rabsha na kujaribu kumshambulia hakimu moja.

Ismael Mustafa, anayedaiwa kumlawiti mvulana mmoja wa umri wa miaka mitatu alizua fujo na kujaribu kumshambulia hakimu mkuu Edna Nyaloti.

Iliwalazimu maafisa wa mahakama kumzuia mshukiwa huyo na kesi hiyo ikaahirishwa.

Kulingana na rekodi za polisi,Mustafa ameshawahi tena kufunguliwa mashtaka ya ulawiti lakini akaachiliwa huru na mahakama kuu baada ya kuwasilisha rufaa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *