Kituo Cha Sanaa Cha Swahili Pot Chapokea Vifaa

Ni habari njema kwa vijana wanaojihusisha na sanaa katika kaunti ya Mombasa hii ni baada ya bodi ya kudhibiti filamu nchini kuweka wazi kuwa inampango wa kuanzisha mashindano kwa wanaojihusisha na sanaa mbali mbali humu nchini.

Akizungumza alipozuru ukumbi wa Swahili Pot hapa mjini Mombasa mkurugenzi mkuu mtendaji wa bodi hio Ezekiel Mutua amesema mashindano hayo ni yakuhakikisha kuwa watu wote wasanaa ambao waliathirika na msambao wa korona wanaweza kujikimu tena kimaisha.

Wakati huo huo Mutua ameweka wazi kuwa sehemu hio ya Swahili pot itawezeshwa zaidi na vifaa vya kisasa ili kuzidi kunufaisha vijana wengi katika eneo hili huku akidokeza kuwa wanamipango ya kuijenga sehemu hio na kuifanya ya kisasa.

Naye msimamizi mkuu wa sehemu hio Mahmooda Noor amesema ipo haja ya wasanii wa hapa Mombasa kuangaziwa nakuwezeshwa ili waweze kufanya vizuri kwenye sanaa yao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *