Kimanzi Ajiuzulu Kama Mkufunzi Wa Harambee Stars

Mkufunzi mkuu wa timu ya taifa Harambee Stars Francis Kimanzi na benchi lake zima la kiufundi wamebwaga manyaga na kuachana na kazi yakuifunza timu hio.

Katika barua kwa vyombo vya habari kutoka kwa shirikisho hilo na iliyotiwa saini na katibu mkuu wa FKF Barry Otieno nikuwa benchi zima la kiufundi likijumuisha mkufunzi Kimanzi, mwalimu wa makipa Lawrence Webo naibu mkufunzi mkuu Zedekia Otieno wamecha kazi rasmi.

Hata hivyo kulingana na arifa hio nikuwa shirikisho hilo halitatoa taarifa nyengine hadi pale mkufunzi mpya atakapoteuliwa.

Itakumbukwa kuwa Francis Kimanzi aliweza kuingota Harambee Stars kwenye mechi ya ushindi dhidi ya Zambia mapema mwezi huu.

Sababu za kikosi hicho cha ukufunzi kuondoka bado hazijawekwa wazi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *