Kilio Chakuhangaishwa Na Wanyamapori Matuga

Wakaazi wa kijiji cha Gopha huko Matuga kaunti ya Kwale wanalalamikia kuhangaishwa na ndovu baada ya  shirika la KWS kushindwa  kuzunguusha ua katika hifadhi ya wanyamapori ya Shimba Hills wanayopakana nayo kwa zaidi ya miaka 10 sasa.
Wakiongozwa na Khamis Fungo wakaazi hao  wanasema kwamba ndovu hao wamewasababishia kukumbwa na baa la njaa kila mwaka kufuatia uharibifu wa mimea yao.
Ni kutokana na mashambulizi hayo yaliyokithiri ambapo takriban Watu 4 wameripotiwa kuaga huku wengine wakiachwa na ulemavu kutokana na ndovu hao wanaovamia makaazi yao nyakati za usiku.
Ramadhan Hamad Mwampanga akisema kwamba wanalazimika kusitisha shughuli zao mapema kwa kuhofia usalama wao.
Sasa wanaitaka KWS tawi la Kwale kuizungishia ua mbuga hio kwa usalama wao na usalama wa chakula

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *