Kilio Cha Umeme Msambweni

Wakaazi wa kijiji cha Kilole kaunti ndogo ya Msambweni wanaendelea kukumbwa na ukosefu wa nguvu za umeme kwa zaidi ya mwezi mmoja na nusu sasa.

Hii ni baada ya mtambo wa kusambaza umeme kuharibika na kukosa kurekebishwa hali ambayo imeleta hasara kwa wafanyibiashara wanaotegemea umeme.

Wakiongozwa na Ali Boi wanasema kwamba wametamaushwa na hatua hio kutokana na kuhangaika kutafuta njia mbadala ya kutafuta bidhaa hio.

Wameitaka kampuni ya Kenya power kushughulikia swala hilo wakisema kuwa wamekuwa na wakati mgumu mno hata kitekeleza biashara zao.

Hata hivyo usimamizi wa Kampuni hio tawi la Ukunda wameahidi kushughulikia swala hilo ili wenyeji wasihangaike.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *