Kilio cha ardhi Mwatate
Wakaazi wa kijiji cha Singila Majengo mjini Mwatate kaunti ya Taita Taveta wamekosoa hatua ya wizara ya ardhi nchini kwa ushirikiano na kampuni ya mkonge ya Teita Sisal kwa kuendelea kukiuka maagizo ya mahakama ya kuzuia shughuli zozote katika ardhi inayozozaniwa.
Wakiongozwa na katibu wa Mwasima Mbuwa Munjala Mwaluma wananchi hao wanadai baadhi ya viongozi katika wizara ya ardhi , wanashirikiana na kampuni hiyo kumnyanyasa mwananchi.
Aidha wamemlaumu pakubwa katibu mwandamizi katika wizara ya ardhi Gedion Mung’aro kwa kuchochea swala hilo akidaiwa kufanya ziara kadha kisiri kaunti ya Taia Taveta, kuzungumzia jinsi ya kusuluhisha matatizo ya ardhi eneo hilo bila hata kuwahusisha wananchi hao.
Hata hivyo ameeleza masaibu mbalimbali wanayopitia dhidi ya bwenyenye huyo wa sisal Estate hali inayowakandamiza kila kuchao
Mwishoni mwa juma Wizara hiyo ilizuru kaunti hii na kuthibitisha kuwa kampuni hiyo imetoa kipande cha ekari zaidi ya mia Saba kwa ajili ya wakaazi wa eneo hilo.