Kilio Cha Ajira Lamu

Wakaazi kaunti ya Lamu wanalaumu serikali kwa kukosa kujumuisha jamii ya eneo hilo katika ajira kwenye mpango wa ujenzi wa bandari wa LAPSET.

Wakiongozwa na Amina Kale Loo ambaye ni mwakilishi wadi mteule katika kaunti hiyo, amesema vijana wametelekezwa katika maswala ya ajira kwa muda mrefu licha ya kuwasilisha lalama kwa usimamizi wa LAPSET.

Kale anadai jamii hiyo imekuwa ikikosa kuhusishwa kikamilifu katika mambo muhimu ya mradi huo unaoendelea katika eneo lao, wakikosoa hatua kuwa wengi ya wanaoajiriwa wanatoka maeneo mengine ya nchi.

Kwa sasa wanaitaka serikali kuzingatia usawa kwa jamii hiyo na kutoa nafasi za ajira kwa vijana wa eneo hilo wakidai vijana wengi kwa sasa wamejiingiza katika uraibu wa mihadarati licha ya miradi muhimu ya serikali kuendeshwa eneo hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *