Kilimo Cha Korosho,Mnazi Na Maembe Kuimarishwa Pwani

Wizara ya kilimo nchini inanuia kufufua kilimo cha nazi, korosho na maembe katika eneo la Pwani kwa kutoa mbegu za kisasa kwa wakulima wa eneo hilo.

Katibu katika wizara ya kilimo nchini profesa Hamadi Boga amesema kuwa tayari wizara hiyo inashirikiana na serikali za kaunti za Pwani katika ukuzaji wa kilimo hicho.

Boga amedokeza kwamba wanapania kuanzisha upya upanzi wa miche ya minazi, mikorosho na miembe ili kuimarisha kilimo hicho katika eneo la Pwani.

Kwa upande wake gavana wa Kwale Salim Mvurya amesema kuwa tayari wanaendelea na mpango wa ugavi wa mbegu zaidi ya laki 5 kwa wakulima wa kaunti hiyo.

Mvurya amefichua kwamba wanashirikiana na taifa la Slovakia katika mpango huo unaolenga kuboresha kilimo cha nazi na korosho.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *