Kidis The Jembe amesema ni basi

Mwanamziki kutoka jiiini Mombasa aliyetamba na ngoma ya “Kamua leo remix” Kidis The Jembe amesema ni basi kufanya mziki.
Mwanamziki huyo ameyasema hayo wakati akiongea na meza yetu ya burudani ambapo amesema dhiki za mziki zimemfanya aache kuimba.
Kidis amedokeza kuwa anahisi kunyanyaswa na kudhulumiwa huku akisema mapato yake ya mziki alistahili kulipwa milioni 1.2 na badala yake akapewa shilingi 124,000 pekee.
Itakumbukwa kuwa alikua chini ya uongozi wa Granpa kabla ya kukosana na uongozi huo kutokana na kutoelewana kuhusu mikataba na malipo ya mapato ya mziki wake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *