Kibe Apewa Majuku Mapya

Mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya safari za ndege humu nchini Gilbert Kibe ameteuliwa kuwa mwenyekiti mtendaji wa  shirika jipya la utoaji  wa huduma za uchukuzi kwa ndege-CANSO.Uteuzi wa Kibe ulitangazwa  kwenye mkutano wa mwaka wa shirika hilo uliofanywa wa njia ya mtandao.Kibe alisema kuwa ameheshimika kuteuliwa kwa wadhifa huo na kuahidi kufanya kazi kwa ushirikiano na wadau wengine duniani ili kulainisha shughuli na kutoa huduma bora  na ilio salama kwa sekta hiyo.Kibe ana tajriba pana ya zaidi ya miaka  30 katika sekta  hiyo,ikiwa ni pamoja na  huduma ya miaka minne kama mwanachama wa shirika hilo jipya.Shirika hilo la CANSO linajumuisha  watoaji huduma 186 kwa usimamizi wa shughuli za uchukuzi kwa ndege na malengo yake ni kuinga mkono na kuifufua  sekta hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *