Kero La Nzige Taita Taveta
Huenda Wakaazi wa maeneo ya Paranga,Ngolia na Ghazi katika eneo bunge la Voi kaunti ya Taita Taveta wakakosa mavuno msimu huu kutokana na uvamizi wa nzige.
Kulingana na wakaazi hao ambao wengi ni wakulima wanasema wamesikitishwa na nzige hao ambao tayari wameharibu mimea yao hasa mahindi.
Wakiongozwa na James Mzaa wanahoji endapo wadudu hao hawatadhibitiwa basi huenda kukashuhudiwa ukame kutokana na mimea kuharibiwa huku wakitoa wito kwa serikali kuingilia Kati.
Kwa upande wake afisa wa mipango katika shirika la umoja wa mataifa la chakula ulimwenguni FAO Abedih Mbatha anasema kuwa wanashirikiana na wizara ya kilimo kaunti ya Taita taveta kutathmini hali halisi katika maeneo yaliyoathirika.
Mbatha anasema kuwa ujio huo wa nzige kwa awamu ya pili huenda umechangiwa na mabadiliko ya hewa nchini.