Kero La Ardhi Kwale

Wakaazi wa Tiwi eneo la  Matuga kaunti ya Kwale wamelalamikia ongezeko la visa vya unyakuzi wa ardhi zao na mabwenyenye katika msitu wa Kaya Tiwi.

Wakiongozwa na Hamisi Majawa, wakaazi hao wameilaumu pakubwa serikali kwa kutowapatia hatimiliki za ardhi zao walizopimiwa zamani.

Aidha, wamepinga vikali hatua ya mabwenyenye kuvamia ardhi zao walizorithi kutoka kwa mababu zao.

Hata hivyo, gavana wa Kwale Salim Mvurya amewaonya mabwenyenye hao dhidi ya kunyakua mashamba ya wakaazi.

Haya yanajiri kufuatia visa vya unyakuzi wa misitu ya Kaya vilivyokithiri katika kaunti hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *