Kenya yanakili idadi ya juu zaidi ya visa vya maambukizi ya corona kwa siku

Kenya ilinakili visa vipya 1,068  vya maambukizi ya Korona na kuongeza idadi jumla  ya maambukizi  hapa nchini hadi 47,212.

Visa hivyo vipya vimetokana na sampuli 7,556 zilizopimwa,hicho kikiwa kiwango cha maambukizi cha asilimia 14.1.

Kwenye taarifa,waziri wa afya Mutahi Kagwe, amesema kati ya visa hivyo vipya ,1,044  ni Wakenya ilhali 24 ni raia wa kigeni.

Kaunti ya Nairobi imeongoza kwa maambukizi kwa kunakili visa 305,ikifwatiwa na Nakuru kwa visa 137 na Mombasa 74.

Hata hivyo wagonjwa 12 zaidi wameaga dunia kutokana na ugonjwa huo,na kuongeza idadi jumla ya vifo kutokana na ugonjwa huo hadi 870.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *