Kenya Power yalaumiwa kwa utepetevu kwale

Wakaazi na mashirika ya kutetea haki za kibinadaam kaunti ya kwale wameandamana hadi katika afisi ya Kenya power eneo la ukunda kuishinikiza serikali kuwapa uhamisho maafisa wa kampuni hio kaunti ya kwale kwa madai ya kuzembea katika utendakazi wao.

Maandamano hayo yanajiri siku chache baada ya mama wa miaka 34 na mwanawe wa miezi 3 kufariki baada ya kupigwa na nguvu za umeme eneo la kombani kufuatia kuanguka kwa kizingiti cha stima na kukosa kushughulikiwa na maafisa wa kenya power kwa zaidi ya wiki mbili.

Wakaazi hao sasa wanadai haki kwa familia sawia na kuboreshwa kwa huduma za usambazaji umeme kwale kwani huduma duni zinazoshuhudiwa zimesambaratisha pakubwa shughuli za kibiashara pamoja na kusababisha hasara kubwa kwa wakaazi wanaotumia vifaa vinavyotegemea umeme katika kaunti hii.

Hata hivyo kampuni ya Kenya power ikiongozwa na mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi Mahboub Maalim amekiri kuwepo na utepetevu katika kampuni hiyo huku akiahidi kuwa tatizo hilo litashughulikiwa ili wenyeji wapate haki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *