Kenya Inamatumaini Yakushamiri Kwenye Mbio Za Half Marathon Za Poland

Mkufunzi mkuu wa timu ya riadha ya Kenya  Patrick Makau anaamini Kenya imechagua kikosi dhabiti ambacho kitatoa ushindani katika mbio za nusu marathon  ambazo zitaandaliwa mjini  Gdynia nchini Poland Jumamosi ijayo.

Kukosekana kwa bingwa mtetezi wa mbio hizo Geoffrey Kamworor  kumetajwa na mkufunzi Makau kuwa hakutataziza kipute hicho kwani orodha ya wakimbiaji ambayo wameichagua itaweza kutoa ushindani wakutosha.

Kamworor pia ni mshikilizi wa dunia wa mbio hizo za marathon amerudi mazoezini baada ya kupata ajali ya pikipiki mjini Eldoret mwezi Juni.

Akizungumza Jumanne jioni kabla ya timu hio kuondoka kuelekea Poland, Makau ambaye ni bingwa wa zamani wa duni katika mbio za marathon ameonyesha kuridhishwa kwake na wanariadha hao akisema watashinda medali kwa taifa la Kenya.

Kenya imeweka matuamaini yake kwa Kibiwot Kandie na mshindi wa nishani ya fedha wa mwaka 2017 katika mbio za dunia za nyika  Leonard Barsoton.

Pia kwenye kikosi ni pamoja na Maurice Munene, Bernard Kipkorir na  Bernard Kimeli.

Peres Jepchirchir ataongoza kikosi chja akina dada pamoja,  Monicah Wanjiru, Jepkorir, Dorcas Kimeli na Joceline Jepkosgei.

Mashindano hayo yaliratibiwa kufanyika mwezi Machi 29 lakini yakahairishwa kutokana na msambao wa janga la korona.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *