KeNHA Yaanza Kutathmini Ujenzi Wa Barabara Kwale

Halmashauri ya barabara nchini KeNHA imeanzisha zoezi la kutathmini hali ya barabara ya Kombani-Kwale _Kinango na ile ya Kinango-Mariakani ili kuona kwamba zinaekwa lami kama ilivyoagizwa na rais Uhuru Kenyatta majuma machache yaliyopita.
Erick Wambua mkurugenzi wa halmashauri hio eneo la pwani anasema ujenzi rasmi wa barabara hizo unatarajiwa kuanza hivi karibuni na kufungua uchumi kusini mwa pwani punde zitakapokamilika.
Aidha ameeleza kwamba wakaazi watakaoathirika na ujenzi huo wa barabara watafidiwa.
Kwa upande wake gavana wa Kwale Salim Mvurya ameelezea kuridhishwa na hatua ya serikali ya kitaifa katika maswala ya utekelezaji wa miradi hio ya barabara.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *