Kaunti Ya Mombasa Kuandaa Mashindano Ya Beach Soccer

Kaunti ya Mombasa inatarajiwa kuandaa mashindano makubwa ya soka la ufukweni mwezi Mei.

Kwenye mazungumzo ya kipekee na pwani fm meza ya michezo  mwenyekiti wa shirikisho la soka ya ufukweni nchini Charlse Juma Kitula ameweka wazi kuwa kwa sasa wakenya wasubiri kuona mchezo huo wa ufukweni kushamiri zaidi kwani kama shirikisho wamejiandaa kuhakikisha talanta za vijana zinakuzwa hususani hapa eneo la pwani.

Kitula amesema kuwa mwezi Mei kaunti ya Mombasa itaandaa mashidano makubwa ya soka la ufukweni ambayo yatajumuisha timu kutoka kila pembe ya Kenya.

Pia amedokeza kuwa mwezi Julai pia kutakua na mashindano ya kimataifa ambayo yatahusisha mataifa ya afrika mashariki.

Kwa sasa kinachotakikana ni bajeti ambayo itfanikisha mashindano hayo huku akisema kuwa wanawataka wafadhili kujitokeza kufanikisha mashindano haya.

Kadhalika amewataka vijana kujitokeza kuanza kushiriki kwenye mchezo huu ambao umeanza kushika kasi humu nchini.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *