Junda Kisauni , Timbwani Likoni na Moroto yameathirika na visa vya wanawake kudhulumiwa
Shirika la Sauti ya Wanawake limefichua kwamba visa 20 vya dhuluma za kijinsia huripotiwa kila siku katika eneo la Mvita pekee.
Ripoti ya shirika hilo inabaini kwamba maeneo ya Junda Kisauni , Timbwani Likoni na Moroto yameathirika sana pia na visa vya wanawake kudhulumiwa
Shirika hilo hata hivyo linasema linasikitika kwamba wanaume wanaodhulumiwa hawajitokezi kuripoti kutokana na unyanyapa huku pia likielezea kwamba limepokea visa kadhaa vya wanaume kudhulumiwa katika msimu huu wa maradhi ya COVID 19.
Ripoti ya shirika la UNECEF linabaini kwamba dhuluma dhidi ya wanawake huongezeka wakati kunapotekea majanga ya aina yoyote .
