Jumwa Kuzuiliwa Hadi Alhamisi

Mahakama kuu ya Mombasa imeagiza mbunge wa Malindi Aisha Jumwa na mlinzi wake Godfrey Okuto waliotarajiwa kufunguliwa mashtaka ya mauwaji hii leo kuzuiliwa katika kituo cha polisi cha Port jijini Mombasa hadi Alhamisi wiki hii.

Akitoa agizo hilo Jaji Njoki Mwangi ametaka wawili hao wawasilishwe katika hospitali ya Rufaa ya Coast General Jumatano ya wiki hii ili kufanyiwa uchunguzi wa akili.

Mwangi pia ameagiza washukiwa hao kuwasilishwa mahakamani 22 mwezi huu kusomewa mashtaka dhidhi yao.

Awali Mkuu wa mashtaka ya umma kwenye eneo la Pwani Alloys Kemo amekinzana na ombili lililotolewa na wakili wa Jumwa na Okuto , Jared Magolo kutaka muda wa wiki mbili ili wateja wake wafanyiwe ukaguzi wa akili.

Kemo ameiambia mahakama hiyo kwamba washukiwa hao walitarajiwa kufika katika hospitali ya Rufaa ya coast general Jumatano wiki iliyopita ili kufanyiwa ukaguzi huo japo wakapuza.

Kemo ameiomba mahakama hiyo kutoa agizo la kuzuiliwa kwa wawili hao hadi Jumatano ambapo watawasilishwa hosptialini kukaguliwa kisha kesi mashtaka dhidi yao yasomwe kuanzia alhamisi wiki hii.

Siku tano zilizopita mkurungenzi wa mashtaka ya umma, Noordin Haji kuidhinisha mbunge huyo kufunguliwa mashtaka hayo.

Ikumbukwe vurungu ziliibuka wakati wa kura ya marudio ya uchaguzi ya eneo wadi hilo ambalo Reuben Katana mjomba wa jola alikuwa akigombea kti kwa tiketi ya odm hatimaye marhemu kuuliwa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *