Jomvu haina maji ya kunywa.

Mbunge wa JomvuBadi Twalib ameihimiza idara ya maji kuhakikisha inagawa maji ya kutosha katika kaunti ya mombasa na viungani mwake badala ya kupitisha maji kuelekea kaunti ya kilifi.

Akizungumza na wanahabari Badi ameukashifu uongozi wa idara ya maji eneo la mazeras na kuihimiza kurekebisha mtiririko wa maji katika eneo la jomvu pia.

Wakati huo huo kiongozi huyo akijibu maswali kutoka kwa waandishi wa habari ameitaka serkali kuhakikisha inazingatia usalama wa wanafunzi wakati huu taifa linapojitayarisha kurejelea shughuli za masomo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *