Jacob ‘Ghost’ Mulee Kuinoa Harambee Stars

Shirikisho la soka nchini humu nchini  Kenya FKF lamteua mkufunzi Jacob ‘Ghost’ Mulee kuionoa timu ya taifa  Harambee Stars kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo, akichukua mahala pa Francis Kiamanzi aliyepigwa kalamu hapo jana.

Mulee sasa atakua na kibarua cha kuionoa timu hio katika michuano ya kufuzu kombe la mataifa ya Afrika nay ale ya kufuzu kombe la dunia mwaka 2022.

Rais wa shirikisho hilo la soka nchini Nick Mwendwa amesema jukumu kubwa ambalo mkufunzi huyo wa zamani wa timu hio ya taifa nikuhakikisha Kenya inafuzu kombe la dunia.

Mulee atasaidiwa na Musa Otieno huku Haggai Azande akipigiwa upato wa kuchukua ukufunzi wa kunoa makipa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *