Idadi ya walioambukizwa homa ya Covid 19 yagonga 16,268

Idadi ya walioambukizwa homa ya Covid 19 nchini imefikia watu 16,268 baada ya wengine 667 katika saa 24 zilizopita.

Akizungumza wakati wa kutoa taarifa ya kila siku katika jumba la afya jijini Nairobi kaimu mwandamizi katika wizara ya afya Dkt. Mercy Mwangangi amesema kuwa watu 657 ni raia wa humu nchini huku 10 wakiwa wa Kigeni.

Kadhalika kaunti ya Nairobi ndio inayosalia kuongoza ikifuatwa na Kiambu kisha Mombasa.

Insert Mwangangi 1

Aidha watu 11 wameripotiwa kufariki kutokana na ugonjwa huo huku 311 wakiwa wamepona.

Kadhalika amewahimiza wazazi kuwa waangalifu kwa watoto wao ili waweze kupata madini ya vitamin D licha ya kwamba wizara ya afya imeagiza watoto wazingatie umbali wa mita moja.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *