Idadi Kubwa Ya Wanafunzi Wamerudi Shuleni Taita Taveta

Hatimaye idadi kubwa ya wanafunzi katika shule kadhaa kaunti ya Taita Taveta wameregea shuleni rasmi hii leo baada ya kulazimika kukaa nyumbani kwa mda mrefu Kufuatia chamko la ugonjwa wa corona

Baadhi ya shule ikiwemo shule ya msingi ya Mwanyambo na shule ya Mwamunga zilizo na idadi kubwa mjini Voi zaidi ya  asilimia 70 ya wanafunzi wa darasa la nne na nane,  tayari wametimiza wajibu wao wa kuripoti shuleni hii leo kulingana na agizo la serikali. 

Akiongea na pwani fm Mwalimu mkuu wa shule ya msingi ya Mwanyambo Livingstone Mlunga ametaja ukosefu wa maji kama changamoto kuu msimu huu wa corona licha ya kujiandaa na mitungi na sabuni kwa ajili ya kutimiza masharti ya wizara ya afya ya kunawa mikono mara kwa mara. 

Hata hivyo uhaba wa madarasa bado ni changamoto kuu kwa shule zote nchini hususan Wanafunzi wote watakaporegea shuleni siku chache zijazo.

Ni swala lililotolewa upato na Mwalimu mkuu wa shule ya msingi ya Mwamunga Mark Mulei iliyoko mjini Voi akihoji kuwa Changamoto hiyo huenda ikalemaza kiegezo cha kuzingatia ukaribu WA mita Moja nusu baina ya wanafunzi 

Hata hivyo wito umetolewa Kwa serikali kupitia wizara ya afya kujizatiti kutimiza ahadi zake kwa shule ili kuboresha miundo msingi sawa na kukabiliana na juhudi za kuzuia maambukizi ya ugonjwa wa corona nchini. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *