Huduma Za Afya Magarini Zatajwa Kudorora

Mkurugenzi wa shirika la KWACHA AFRICA katika eneo la Magarini kaunti ya Kilifi Evans Kasena ametaja huduma za zahanati katika eneo la Sosoni wadi ya Marafa katika eneo hilo kuwa duni 
Akizungumza katika halfa ya kuwasilisha baadhi ya maswala yaliyojiri baada ya shirika hilo kupata maoni kwa baadhi ya wananchi katika eneo hilo kuhusiana na huduma wanazozipokea katika zahanati hiyo Evans ameelezea kutokuwepo kwa maafisa wa afya wakutosha katika zahanati hiyo kama moja wapo ya maswala yanayochangia kudorora kwa huduma hizo.
Mkurugenzi huyo ameeleza kuwa zahanati hiyo imekuwa ikitumia bima ya serikali inayosimamaia gharama za kina mama kujifungua ya LINDA MAMA kulipia baadhi ya wauguzi katika zahanati hiyo huku akina mama wakilazimika kugharamikia huduma za uzazi pale wanapo jifungua.
Hata hivyo mwakilishi wa wadi eneo hilo Renson Karisa ameonekana kugadhabishwa na hatua hiyo na kumtaka msimamizi wa wizara ya afya katika kaunti ndogo ya Magarini Hossan Ajuk kuingilia kati na kutatua huku akimpatia makataa ya wiki moja kuafikia hilo. afya katika kaunti ndogo ya Magarini Hossan Ajuk kuingilia kati na kutatua huku akimpatia makataa ya wiki moja kuafikia hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *