Hofu Yakufurushwa Mwatate

Wakaazi wa Mwakitau eneo bunge  la Mwatate Kaunti ya Taita Taveta Sasa wanaishi kwa hofu ya vurugu kufuatia mzozo  wa ardhi baina yao na vuguvugu moja linalojiita isanga iwishi.

Wakaazi hao Sasa wameitaka Serikali kuingilia kati swala hilo na kutoa suluhu mwafaka dhidi ya utata huo ambapo wanalaumu vuguvugu la Isanga iwishi linalotaka kuwafurusha, kwa madai kuwa ndiyo wamiliki halisi wa eneo hilo licha ya Wakaazi hao kuishi katika sehemu hiyo kwa zaidi ya karne moja Sasa.

Kadhalika wameilaumu vuguvugu la Isanga iwishi kwa kutumia mradi wa ujenzi wa chuo kikuu Katika eneo Hilo la Mwakitau, Kama chambo Cha kuwafurusha Wakaazi hao huku wakilaumu idara husika sawa na baadhi ya wanasiasa kwa kushindwa kusaka suluhu mwafaka.

Ikumbukwe idadi kubwa ya Wakaazi hao walijitokeza Jumamosi uliyopita kuandamana  ili kulalamika na kupinga dhuluma ya unyakuzi wa ardhi zao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *