Harambee Stars Kupambana Na Chipolopolo Ya Zambia

Aliyekua kiungo wa timu ya AFC Leopards Francis Xavier amedokeza kuwa timu ya taifa Harambee Stars lazima ijikakamue zaidi ili kuipiku timu ya taifa ya Chipolopolo ya Zambia kwenye mchezo wa kirafiki siku ya Ijumaa.

Kenya itaikaribisha Zambia Oktoba 9 mwaka huu ugani Nyayo ambapo kipute kikali kinatarajiwa mtanange huo ambapo takwimu zikionyesha kuwa Zambia imekua ikiitawala Kenya kisoka tangu timu hio zikutane kwenye mashindano ya kombe la bara Afrika mwaka 1964.

Kwa upande mwengine Zambia wachezaji wao wametajwa kua bora zaidi kwa sasa ikizingatiwa kuwa ligi yao ilirejelewa baada ya kusimamishwa kutokana na janga la korona huku ligi ya Kenya ikiwa bado haijaanza tena tangu kusimamishwa manmo mwezi Machi.

Kwa sababu hio Xavier amesema ni lazima Kenya ijiweke vizuri kuikabili Chipolopolo.

Wakati huo huo Xavier ametaja kukosekana kwa wachezaji  Michael Olunga, Victor Wanyama, Ayub Timbe, Arnold Origi na Johana Omollo kwa kiasi Fulani kutaathiri timu hio.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *