Hali ya mgomo wa wahudumu wa afya Nigeria

Wahudumu wa afya nchini Nigeria wamesitisha mgomo wao.

Mgomo huo ulianza kati kati ya mwezi huu kushinikiza kuboreshwa kwa mazingira ya kazi,malipo ya malimbikizi ya mshahara na marupurupu ya kukabiliana na janga la Korona.

Chama cha wahudumu hao sasa kimewashauri wanachama wake kurejea kazini kuanzia siku ya jumatatu ijayo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *