Guinea Yaonywa Kuhusu Kuenea kwa Chuki Wakati wa Kampeni

Umoja wa Mataifa umeonya kwa uhasama wa kijamii na uenezaji jumbe za chuki wakati wa kampeni za uchaguzi nchini Guinea; huenda vikasababisha mapigano. Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu haki, Michelle Bachelet, na Kaimu mshauri maalum kuhusu udhibiti wa mauaji ya halaiki Pramila Patten, wamewahimiza wagombezi kwenye uchaguzi huo kutotoa hotuba za chuki. Rais Alpha Condé anayewania  hatamu ya tatu, anaungwa mkono na watu wa jamii ya Malinké ilihali mpinzizani wake mkuu, Cellou Dalein Diallo, anaungwa mkono wa jamii ya Fulani, ingawaje wote wanadai kuwa na ufuasi mkubwa. Uchaguzi wa Urais nchini Guinea utaandaliwa tarehe-18 mwezi huu. Kufikia sasa, watu 50 wameuwa kwenye maandamano ya kupinga hatua ya Rais Condé  kuwania hatamu ya tatu ya Urais.

Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu haki, Michelle Bachelet Aonya Wagombezi wa urais Guinea dhidi ya Kutoa hotuba za uchochezi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *