Gavana Joho Afadhili Matibabu Ya Msanii Bin Kalama

Msanii wa nyimbo za kitamaduni kutoka hapa mjini Mombasa Bin Kalama ambaye anatambulika sana na kutamba na nyimbo zake za kitamaduni  amepata ufadhili wa kimatibabu kutoka kwa gavana wa kaunti ya Mombasa Hassan Joho na anasafiri hadi Nairobi katika hospitali ya Kijabe kufanyiwa matibabu ya mkono wake ambao umekua ukimsumbua kwa muda sasa.

Akiongea na meza yetu ya burudani Bin Kalama amesema kwa muda sasa amekua akizunguka akitafuta matibabu hali ambayo imemfanya kukwamisha shughuli zake za kilasiku.

Bin Kalama amedokeza kuwa hali yake haijazorota ila amechukua tahadhari zaidi ili kutibu tatizo ambalo amesema lingekuja msumbua mbeleni.

Msanii Susumila kupitia ukurasa wake wa Facebook ameweka wazi safari ya Bin Kalama huku akiwaomba mashabiki kumukumbuka kwa maombi msanii Bin Kalama.

Kwa sasa msanii huyo ambaye anatajwa kuwa mmoja wa wasanii wa kimijikenda ambaye anamafanikio makubwa kutokana na mziki wake anatamba na kibao chake kipya cha korona  ambacho amesema alikitunga wakati akiwa hospitali akipokea matibabu.

“Wimbo wa korona niliuimba nikiwa hospitalini Mkadara na licha ya kuwa nilikua naumwa niliamua kutoa ujumbe huo wakuwahamasisha wakenya dhidi ya kujikinga na maradhi ya korona”. Amesema Bin Kalama.

Msanii huyo amemshukuru sana gavana Joho akimtaja kama mtu mkarimu ambaye amechukua jukumu ambalo wengi wameshindwa kujitwika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *