Fuo za bahari kufunguliwa.

Idara ya usalama hapa Mombasa inasema inatathimini mikakati ya kufungua rasmi fuo za bahari kwa umma baada ya kufungwa kwa muda kutokana na maambukizi ya homa ya Covid 19.

Kamishna wa kaunti ya Mombasa Gilbert kitiyo anasema wanajadiliana na kamati maalumu iliyotwikwa jukumu la kuangazia maambukizi ya corona kabla ya ufunguzi rasmi.

Kitiyo anasema utekelezaji wa masharti ya kukabiliana na kusambaa kwa maradhi ya virusi hivyo, yatapewa kipaumbele kabla ya ufunguzi wa sehemu hizo za umma.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *