Familia 400 zaachwa bila makao Lamu

Zaidi ya familia 400 katika eneo la Mukowe kaunti ya Lamu zinalilia haki baada ya ardhi yao ya zaidi ya ekari 100 kutwaliwa na serikali ya kaunti hiyo bila ya kuwahusisha.

Wanadai imepita zaidi ya miaka nane tangu unyakuzi huo wa ardhi kutekelezwa na maafisa wa serikali ya kaunti ya lamu,japo juhudi za kufidiwa au kurejeshewa ardhi hiyo zimegonga mwamba licha ya wao kukita kambi kwenye ofisi ya gavana wao kutafuta  haki.

Sasa familia hizo zinaitaka serikali ya kitaifa kuingilia kati ili kuona kuwa wanapata haki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *