Everton ipo tayari kumwachilia Moise Kean

Mkufunzi wa timu ya Everton, Carlo Ancelotti, amesema kuwa timu hiyo iko tayari kujadiliana na Paris Saint-Germain kuhusu uhamisho wa Moise Kean, ikiwa mshambulizi huyo anaazmia kusalia nchini Ufaransa.

Kean alijiunga na PSG kutoka Everton kwa mkopo mwezi Oktoba mwaka jana, na mapema mwezi huu ripoti zilidai kuwa mabingwa hao wa Ufaransa wameanza majadiliano kuhusu kumsajili kwa kima cha pauni milioni 31.

Mkufunzi Mauricio Pochettino, aliyejiunga na PSG hivi majuzi, anadai kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20, huku akiwa amefunga mabao 11 katika mashindano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya na ligi kuu nchini Ufaransa.

Raia huyo wa Italia amenawiri jijini Paris, huku akicheza kwenye safu ya ushambulizi pamoja na Neymar na Kylian Mbappe, ikilinganishwa na alipokuwa akiiwakilisha Everton ambapo alifunga mabao manne pekee katika mechi 37.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *