Ethiopia yataka ufafanuzi kuhusu ufadhili wa bwawa la Gerd

Serikali ya Ethiopia imetaka ufafanuzi kutoka Amerika kuhusu ripoti kwamba imepunguza ufadhili wake kwa Ethiopia huku mzozo ukiendelea kuhusiana na bwawa la Grand Ethiopian Renaissance (Gerd).

Balozi wa  Ethiopia nchini Marekani Fitsum Arega amesema kupitia mtandao wa tweeter kwamba Amerika imesema itaelezea uamuzi huo hii leo.

Lakini haijathibitishwa iwapo ufadhili huo umekatizwa.

Wiki jana jarida moja liliripoti kuwa waziri wa mashauri ya kigeni wa Amerika Mike Pompeo aliidhinisha kusitihswa kwa msaada wa dola milioni 130 kwa Ethiopia katika juhudi za kuishurutisha nchi hiyo kuafikiana na Misri kuhusu bwawa hilo la Renaisance.Kwa takriban miaka kumi sasa,Misri na Ethiopia zimekuwa zikizozana kuhusu bwawa hilo kwenye mto Nile.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *