Ethiopia Kukabiliana na Nzige Kutumia Ndege

Waziri wa kilimo nchini Ethiopia, Oumer Hussien, amesema serikali itapeleka ndege zaidi za kunyunyiza dawa ili kukabiliana na nzige wanaoharibu mimea. Hii ni baada ya ndege mbili zilizokuwa zikitumiwa kwa kazi hiyo kukwama mapema mwezi Oktoba na kudidimiza juhudi za kuangamiza wadudu hao. Waziri huyo alisema Nzige wamesambaa hadi mikoa Minne, na wanatishia hali ya taifa hilo kujitegemea kwa chakula.Aliongeza kwamba wizara hiyo iko kwenye mchakato wa kuwatambua wakulima walioathirika zaidi na uvamizi huo na kuwapa usaidizi.Nzige walionekana katika mataifa kadhaa ya ukanda wa Afrika mashariki ambapo waliharibu mimea.Wataalam wameutaja kama uvamizi mbaya kuwahi kutokea kwa takriban miaka 60 hivi.

Ethiopia Yatangaza kukabilana na Nzige kutumia ndege

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *