Spika wa Bunge la Nairobi Elachi ajitetea

Spika wa Bunge ya Kaunti ya Nairobi Beatrice Elachi amekana madai ya kushabikia vitendo vya polisi dhidi ya wawakilishi wadi.

Hii ni baada ya video kusambaa katika mitandao ya kijamii akiskika akiwatia motisha kuwaadhibu wawakilishi hao.

Elachi ameelezea kusikitishwa na vitendo vya siku ya jumanne katika bunge la kaunti hiyo na kusema kuwa ni vita kati ya Gavana Mike Sonko na Msimamizi wa jiji la Nairobi Generali Abdallah Badi.

Kuhusu tamko la Waziri wa usalama wa ndani la kama angekuwa na uwezo angelivunja bunge la kaunti ya Nairobi kutokana na fujo za kila mara,Elachi amesema swala kuu ni kuangazia matatizo ya Nairobi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *