Diego Maradona Afariki

Aliyekuwa mchezaji wa soka wa timu ya taifa ya Argetina Diego Maradona amefariki akiwa na umri wa miaka 60 wiki mbili baada ya kuruhusiwa kuondoka hospitalini baada ya kufanyiwaupasuaji.

 Maradona alikuwa na tatizo la kutokwa na damu kwenye ubongo na mapeama mwezi huu alifanyiwa upasuaji katika hosptali moja mjini Benous Aires nchini Argentina.

Nguli huyo wa soka alishinda kombe la dunia na taifa laArgetina mwaka wa 1986 na atakumbukwa sana kutokana na bao lake dhidi ya Ungereza  alamarufu “hand of God”bao liloisaidia Argetina kuwabandua Ungereza nje ya dimba hilo.

Kando na kuwa mchezaji bora uwanjani maisha yake Maradona nje ya uwanja pia yalija vioja si haba ikikumbukuwa kuwa aliandamwa na kesi za madawa ya kulevya na utumizi wa pombe kupita kiasi.

Maradona alikuwa na watoto wawili Gianinna na Dalma.

Gianinna alikuwa ameolewa na Sergio Aguero toka mwaka wa 2008-2012 kabla ya kutengana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *